January 28, 2016

FACEBOOK YAANZA MWAKA 2016 KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

Facebook

kampuni ya mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza ongezeko kubwa la mapato na faida, miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2015, faida iliongezeka mara mbili zaidi ya dola bilioni moja na nusu ukilinganisha na mwaka 2014 katika kipindi kilekile.

Hisa ziliongezeka kwa saa baada ya kufanya biashara mjini new york na kupata kukidhi matarajio yao. Facebook kwa sasa imevuka kiwango ambacho wachambuzi wa masuala ya biashara walichokuwa wanakitarajira zaidi ya mara kumi katika kipindi cha miezi mitatu.

Kampuni hii iliyoko Califonia inasema watu wengi walikuwa wanatumia simu zao za mkono ili kuangalia tovuti zao na kupelekea kiwango cha asilimia themanini ya mapato katika sekta ya matangazo

Source:bbc


By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.