Featured Posts

January 14, 2016

GOODLUCK GOZBER AACHIA ALBUM MPYA 'IPO SIKU'


Muimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki, Goodluck Gozbert ambaye pia anafahamika kwa jina la Lollipop ameachia rasmi album yake mpya iitwayo ‘Ipo Siku’.

Goodluck ambaye mwishoni mwa mwaka 2015 alishinda tuzo ya ‘Wimbo Wa Mwaka’ kwenye Xtreem Awards za nchini Kenya, amesema album yake yenye nyimbo nane (8) imeingia sokoni Alhamisi ya January 14, 2016 na inasambazwa na kampuni ya Msama Promoshens.


Miongoni mwa nyimbo zinazopatikana kwenye album hiyo ni pamoja na ‘Ipo Siku’ na ‘Acha Waambiane’ ambazo ziliachiwa kwenye vituo vya redio toka mwaka jana. Nyingine ni ‘Hao Hao’, ‘Nimesamehe’, ‘Pendo Langu’, ‘Moyo Tulia’ na ‘Surprise’.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.