January 4, 2016

KAGAME KUGOMBEA MUHULA WA 3, MAREKANI YAKERWA.


Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa tatu wa Urais baada ya wananchi kupigia kura rasimu ya katiba inayomruhusu kufanya hivyo.

Akihutubia taifa hilo siku ya mwaka mpya, Kagame alidai kuwa uamuzi wake huo umetokana na chaguo la wananchi wake.

Wananchi wa Rwanda waliipigia kura rasimu ya katiba hiyo  December 18 kumruhusu Kagame, 58, kuwania tena muhula mwingine wa urais mwaka 2017 wenye miaka saba.

Katiba hiyo itamruhusu kuwania tena mihula mingine miwili ya miaka kumi hadi mwaka 2034.

Hata hivyo Marekani imelaani vikali hatua hiyo.


"The United States is deeply disappointed that President Paul Kagame has announced his intention to run for a third term in office" maelezo ya serikali ya Marekani yalisema.

By Chief Hope

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.