January 15, 2016

KANISA LENYE UMBO LA KIATU LAJENGWA TAIWAN.

Kanisa la urefu wa mita 16 lililojengwa kwa kutumia vigae vya glasi linalofanana na viatu vyenye visigino virefu vinavyopendwa sana na wanawake limejengwa huko Taiwan kwa lengo la kuwavutia wanawake zaidi.

Soma: Picha Za Ghorofa (Jumba Jipya) La Askofu Dastan Maboya.

Likiwa limejengwa kwa kutumia vigae vya glasi takriban 320,kanisa hilo la rangi ya buluu lina upana wa mita 10 na limegharimu takriban dola 686,000.
Picha iliopigwa juu ya kanisa hilo pia imeonyesha ukubwa wa kanisa hilo pamoja na uzuri wa eneo lililojengwa.
Jumba hilo la kuabudu lililo-funguliwa tarehe 8 mwezi Februari.

Kiatu hicho kimetengezwa na maafisa wa baraza la miji kusini magharibi mwa pwani ,katika eneo moja la kitalii lenya umaarufu mkubwa huko Taiwan.

Soma: Raila Odinga Aanguka Jukwaani Alipokuwa Akisimulia Kuhusu Mateso Aliyopitia Yesu Kristo. (+video)

Lakini Pan Tsuei-ping, msimamizi wa ujenzi huo, ameiambia BBC kwamba kanisa hilo halitatumika kwa huduma za ibada za kila siku bali hafla za harusi.

''Katika mipango yetu, tunataka kulifanya eneo hili kuwa la kuvutia kimapenzi, kila msichana angepanda kutafakari atakapokuwa bibi harusi alisema'', Pan aliiambia BBC.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.