• Isikupite Hii

  January 16, 2016

  MASANJA AELEZA KUHUSU BMW X6 YAKE NA MAGARI MENGINE ANAYOMILIKI.

  Gari aina ya Bmw X6. Picha husika iko chini hapo.
  Mchekeshaji wa Orijino Komedi, mjasiriamali, mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Masanja Mkandamizaji amesema kila anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye plate namba ya jina lake.

  Soma: Picha 4 Za Mishe Mishe Za Masanja Mkandamizaji Akisaka Pesa Mtaani.

  Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV, Masanja alisema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli. 
  Masanja akiwa na Bmw X6 Yake.
  "Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine," alisema. 

  Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,” alijinadi. 

  Aliongeza, “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia.” 

  Soma: Masanja Alivyo-mvunja Mbavu Mhe Magufuli Ikulu.(+video)

  Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu. 

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
   
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.