• Isikupite Hii

  January 7, 2016

  RAIS OBAMA AANGUSHA MACHOZI ALIPOKUWA AKITOA HOTUBA. KISA NINI? (SOMA HAPA + VIDEO)


  Ishu ya matukio mfululizo ya mauaji Marekani yakihusishwa matumizi ya silaha yamekuwa yakitawala vichwa vya habari za Marekani na duniani.. mjadala ukaibuliwa kwamba kuna sababu zote za msingi itengenezwe sheria ya kudhibiti matumizi ya silaha.

  Japo kumekuwa na mvutano mkubwa kuhusu Bunge la Marekani kupitisha sheria hiyo, jana January 5 2015 Rais wa Marekani alijikuta akitokwa machozi wakati akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuwa na sheria kali za kudhibiti umiliki na matumizi ya silaha.

  Rais Obama anakaribia kumaliza kipindi cha uongozi wake huku akionesha kuwa hili la sheria za silaha ni la msingi zaidi kumalizana nalo kabla hajatoka.

  Video yake hii hapa pia dakika mbili za Rais Obama kwenye hotuba yake.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.