January 11, 2016

KONGAMANO LA KUOMBEA TAIFA NA VIONGOZI KUANZA LEO.Mkoa wa Dodoma, leo unatarajiwa kufanya kongamono la siku tano la kuombea taifa pamoja na viongozi, ambalo pia litawashirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini na wa serikali.

Katibu wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma, Askofu Dk. Eliya Mauza, alisema kongamano hilo limeandaliwa na Nyumba ya Maombi Taifa kwa kushirikiana na Umoja wa Madhehebu ya Kikristo mkoani Dodoma.

Dkt Mauza alisema lengo la kongamano ni kuiombea serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Dk. John Magufuli pamoja na Baraza la Mawaziri ili iweze kufanya kazi zake chini ya ulinzi wa Mungu.

“Lengo la kongamano hili ambalo viongozi wake wanatarajia kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, ni kuombea taifa na viongozi wetu wa kitaifa ikiwemo na Zanzibar ambayo mpaka sasa iko kwenye mvutano wa kumpata rais wake,” alisema.

Katibu huyo wa umoja alisema kuwa kongamano hilo pia litachukua kipindi hicho kuombea Umoja wa Makanisa ya Tanzania kutokana na kutokuwa na ushirikiano wa kiroho na kimwili.

Source: Nipashe.


By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.