January 13, 2016

R4C WALEJEA TENA NA HII NDIO KAZI YAO MPYA.


Baada ya R4C kutoa hit song "Am Confident" ambayo ndio inayoongoza kwa downloads kuliko nyimbo zao nyingine zote, na kutulia kwa mda mrefu bila kusema wala kufanya chochote kile, sasa R4c wamelejea tena kambini, na wametangaza kuachia wimbo mpya hivi karibuni "Thankfull".

Wamesema wimbo huo ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu na kutazama yote ambayo ameyatenda na anayotenda katika maisha yetu ya kila siku. 

"Mungu anastahili kupewa sifa, kuna wakati Mungu anatenda mambo kwa ajili yetu na tunadhani kwamba labda ni jitihada zetu mwenyewe ama ni bahati tumepata. Yote hayo ni sehemu ya mpango/mipango mikubwa ambayo Mungu amepanga kwa ajili yetu" Alisema Da Gower ambae ndie kiongozi wa kikundi hicho cha R4C "Representative For Christ"  

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.