Featured Posts

January 6, 2016

MTANDAO WA TWITTER KUBORESHA HUDUMA ZAKE. (SOMA HAPA)


Mtandao wa kijamii wa Twitter inasemekana una mpango wa Kuongeza kikomo cha idadi ya maneno wakati wa Ku-tweet ‘character limit’ na kufikia maneno 10,000 kwa tweet moja.

Ripoti zinasema mpango huo mpya utatumika pia na kwenye ujumbe wa moja kwa moja – DM (Direct Message) ambapo sasa mtumiaji wa Twitter atakuwa na uwezo wa kutuma DM yenye maneno elfu kumi kwenye ujumbe mmoja.

kwa sasa Twitter inaruhusu mtu kuandika maneno yasiyozidi 140 kwenye kila tweet moja.

Inasemekana mpango huo unaweza kuanza kutumika ifikapo mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka huu 2016. Twitter wenyewe bado hawajathibitisha chochote mpaka sasa.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.