• Isikupite Hii

  January 19, 2016

  SHANGWE AFUNGUKA 'WATU WANATUSUMBUA SANA SISI WAIMBAJI WA KIKE NA KUTUTAKA KIMAPENZI.


  Shangwe Phostiny Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania amesema kuwa changamoto kubwa anayokutana nayo kama mwimbaji msichana (maarufu) ni watu wengi kumtaka kimapenzi. 

  Akiongea na SirMbezi Shangwe amesema hilo ni tatizo kwa kuwa wakati yeye anawaza kufanya kazi na watu fulani wao wanawaza mambo mengine.

  Nilipotaka kujua kama mwanadada huyo ana maono ya kuolewa na kwanini aone ni usumbufu ikiwa vitu kama hivyo si vigeni kwa mtoto wa kike, Shangwe alikiri kuwa ana maono ya kuolewa lakini jinsi watu wanavyokuja ndio tatizo.

  “Sijui kwa kuwa unaonekana sana kwa watu! maana hali hii imezidi..mwingine anataka tu akujaribu aone ukoje, mtu mwingine akukwaze tu” alifunguka Shangwe Phoustine ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 21.

  “Ni kweli mimi ni msichana na nina maono ya kuolewa, lakini watu waje kistaarabu. Unakuta mtu ana mke, familia na watoto halafu anakutaka na wewe pia, mtu kama huyo ana maanisha nini?” aliongeza Shwangwe ambaye kwa sasa ana album inayokwenda kwa jina la "Utukufu umeshuka".

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.