Featured Posts

February 16, 2016

BONDIA MANNY PACQUIAO AKEMEA NDOA NA WAPENZI WA JINSIA MOJA.

Bondia Mfilipino Manny Pacquiao asema kuwa wapenzi wa jinsia moja ni 'watu wabaya hata zaidi ya wanyama'. 

Katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye runinga ya kitaifa bondia huyo ambaye pia ni mwanasiasa alizua mjadala mkali na majibizano kati ya wanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja na umma. 
Bondia huyo bingwa wa zamani wa uzani wastani duniani ni mkristo imara ambaye anawania kiti cha useneta katika uchaguzi mkuu ujao unaoratibiwa kufanyika mwezi Mei. 

Ufulipino ina asilimia kubwa ya wakatoliki ambao wanapinga kimya kimya mapenzi ya jinsia moja. Mbunge huyo ( Pacquiao), alikuwa akihojiwa katika runinga ya TV5 mapema hapo jana. 

Video inayoonesha wakati alipotamka maneno hayo katika lugha ya Tagalog, inamuonesha bondia huyo akisema. 

"Ni ukweli usiopingika kuwa wanyama ambao tunawafuga wanaheshimu maadili ya kiume na ya kike, Je ushawahi kuona mnyama wa kiume akimkurubia mwenzake wa kiume? Au hata mnyama wa kike akimpandilia yule wa kike? Haiwezekani, Kwa hivyo wanadamu wamegeuka na kuwa wabaya hata kuwazidi wanyama"

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.