February 12, 2016

JIONGEZE MWAKA 2016 PIGA CHINI WASIOKWENDA NA WEWE - SAM SASALI.

Kama Unasafiri unaenda Arusha huwezi Jichanganya na abiria wa Mbeya ukifika pale Stend ya Mabasi Ubungo kwa wakazi wa jiji la Dar. Kama unaenda Mtwara ama Lindi huwezi kwenda Ubungo utaenda Mbagala.

Kama Unaenda Na Ndege ukifika Airport kuna abiria wa ndani na abiria wa nje, na kila abiria anaondoka na ndege yake na muda wake na kila mtu ana Seat yake na kila mtu ana namba ya Seat yake. Ukiwa unaenda Zanzibar hauendi Stend ya mabasi Ubungo. Kila safari ina kituo chake, ina watu wake na usafiri wake.

Unaweza shangaa unafika kituo chako cha safari ukashangaa kuna watu wengiii ukadhani umekosa tiketi kumbe wengi ni Wasindikizaji tu. Unaweza kuta mtu mmoja amesindikizwa na watu kumi. Sio kila mtu ni Msafiri wengine ni wasindikizaji.

Kwanini unakaa na watu ambao hamuendi safari moja ya maisha? kwanini unang'ang'ania kupanda na mabegi mazito ndani ya gari wakati kuna Buti za gari? Mwaka 2016 umeanza umeyabeba mambo mazito ya mwaka 2015, umebeba mizigo ya watu, mawazo ambayo inakulemea kupiga hatua za maisha. Kuna Mizigo hutakiwi kuibeba kuna watu hutakiwi kuwabeba unapaswa kukutana nao mwisho wa safari. Mzigo wa kwenye buti unapaswa kuuchukua mwisho wa safari.

Usikazane kuwa na marafiki wasiokwenda safari moja na wewe, usiwabebe watu ambao hamuendi safari moja na wewe ya maisha hata kama ni Mpenzi wako. Usibebe vitu vinavyopunguza speed ya kuelekea kilele cha mafanikio yako. Unajikuta muda mwingi unawaza vitu unawaza watu unawaza ulivyoumizwa unawaza ulivyopata hasara.

Hakikisha unasafiri na watu sahihi hakikisha unaenda kituo sahihi na Class sahihi. Ukitaka kupanda First Class lazima ulipe gharama.

Maamuzi yako yanayotegemea watu wenye akili mnazo fanana mtaamua mambo yale yale namna ile ile na matokeo yatakuwa yale yale. Jiongeze mwaka 2016 piga chini wasiokwenda na wewe.
Think Differently, Make a Difference.


Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.