February 12, 2016

EXCLUSIVE: GELAX WA KRISTO NA 'KUJIKANA'.


Gelax wa KRISTO afunguka vyema kuhusu wimbo wake mpya 'KUJIKANA'. 

"Kujikana - ni kumpa na kumuachia YESU atawale maisha yako kwenye kila Nyanja kwa Nia, Kimawazo na mipango ya kutimiza kusudi, kwa kuruhusu moyo wako kumwamini na kumshuhudia kwa maneno ya kinywa.
INJILI ni mbegu iliyohai, inayozaa ukiiweka kwenye matendo na kuieneza Habari Njema uliyoiamini nakukubadilisha bila kutazama wadhifa,hadhi,cheo,heshima,umaarufu,Utashi na kujishusha kana kwamba wewe si lolote pasipo KRISTO.
Kutokuendekeza mwili kwa matakwa yake bali kufuata roho inayohitaji uzima wa sasa na baadaye ni KUJIKANA kwa Ajili ya YESU KRISTO naye atakuthibitisha mbele ya BABA aliye mbinguni." Alisema Gelax.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.