February 19, 2016

INDIA YATENGEZA ‘SMARTPHONE’ YA BEI RAHISI DUNIANI, INAUZWA DOLA 3 SAWA NA TSH 6300 (+PICHA)

Kampuni moja ya India inatarajiwa kuzindua kile kinachojulikana kuwa simu aina ya smartphone ya bei rahisi.

Kampuni ya Ringing Bells imesema kuwa simu hiyo kwa jina Freedom 251 itagharimu Rupee 500 sawa na dola 7.3, lakini vyombo vya habari nchini India vimesema kuwa itauzwa kwa Rupee 251 pekee ambazo ni sawa na dola 3.67.
Ripoti zinasema simu hiyo ina ukubwa wa 8GB na ina kamera mbele na nyuma. India ni soko la pili kwa ukubwa la simu na lina wateja bilioni moja wanaomiliki simu. 

Freedom 251 inatarajiwa kulenga soko ambalo tayari linatawaliwa na simu za bei ya chini.
“Hii ndio modeli yetu ya kwanza na tunafikiri kwamba inaleta mabadiliko katika soko la simu, Kwa sasa kampuni hiyo inanunua vifaa vya kutengezea simu kutoka nje kabla ya kuviunganisha nchini India,lakini ina mpango wa kutengeza vifaa hivyo nchini India katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.” shirika la habari la AFP, lilimnukuu msemaji wa kampuni hiyo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.