February 24, 2016

Video ya wapenzi wa jinsia moja marufuku kenya..

Bodi ya kudhibiti video na filamu nchini Kenya (KFCB) imepiga marufuku video moja ya muziki inayotetea haki za wapenzi wa jinsia moja.

Bodi hiyo inasema kuwa video ya ''wimbo huo inakiuka maadili ya jamii''. Wimbo huo wa "Same Love (Remix)" ni chapa ya wimbo wa awali ulioimbwa na Macklemore na Ryan Lewis mwaka wa 2012.

"Same Love'' unatambulishwa kama wimbo unaotetea maslahi ya wapenzi wa jinsia moja katika anuani yake ya mtandao wa video wa Youtube.

Katika video hiyo iliyochapishwa yapata juma moja lililopita na kutazamwa na takriban mara elfiu arobaini katika mtandao wa Youtube.

Haijulikani kwa njia gani bodi hiyo itatekeleza marufuku yake.
Mkurugenzi wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alitangaza marufuku hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter.