• Isikupite Hii

  February 10, 2016

  MACHALII WA YESU KUACHIA WIMBO MPYA VALENTINE'S DAY.

  Machalii wa Yesu kutokea Arusha wamejipanga kuachia wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Yesu anakupenda ambao uko kwenye mahadhi ya HipHop na umefanywa na vichwa takribani nane vya muziki huo.

  Wimbo huo ambao umefanyika chini ya producer Sam Timber kutoka Fnouk studios unatarajiwa kuachiwa siku ya Valentine,tarehe 14/02/2016.

  Katika kuelekea kwenye siku ya kuachiliwa kwa wimbo huo, Machalii wa Yesu wanakuletea Yesu anakupenda Challenge ambapo mashabiki na wadau watapewa nafasi ya kuotea hao watu wanane walioshiriki kwenye wimbo huo kwa kuwatambua kutokana na wasifu wa kila mmoja utakaokuwa ukitolewa kwenye ukurasa wa facebook wa Machalii wa Yesu.
  Machalii wamejipanga kuwapongeza watu wa kwanza kuweza kuotea watu hao.

  Ungependa kushiriki?Tembelea ukarasa wao wa facebook ambao ni Machalii wa Yesu kisha fuata maelekezo 

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.