February 5, 2016

MASANJA MKANDAMIZAJI KUFUNGUA KITUO CHAKE CHA RADIO NA TV.

Mwimbaji wa nyimbo za injili na mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji ameweka wazi mpango wake wa kufungua kituo cha Radio na TV ambavyo atavisimamia yeye mwenyewe.

Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm Alhamisi hii, Masanja alisema tayari ameshapata mafunzo ya uandishi wa habari ili kujifunza kuhusu kuendesha vituo hivyo.

"Yeah nimepanga kufungua kituo changu cha radio na TV," alisema Masanja.

"Nilikuwa na mpango wa muda mrefu ndio maana nikaenda shule ili kujifunza mambo mbalimbali kusuhu uendeshaji. Sasa hivi niko poa kabisa, najua vitu vingi hata nikiwaajiri watu hawata nidanganya kwa sababu najua kila kitu," 

Masanja licha ya kuwa ni muigizaji na mfanyabiashara, pia ni mkuliwa mkubwa wa zao la mpunga.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.