February 23, 2016

Rais Mugabe atimiza miaka 92.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza umri wa miaka 92 huku chama chake kikisema atawania tena urais 2018.

Mnadhimu wake mkuu alisema kiongozi huyo ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 1980, bado ana uwezo kamili wa kuongoza Serikali licha ya tetesi kwamba hawezi kuongoza kutokana na umri.

Keki hiyo ilikabidhiwa bwana Mugambe katika sherehe iliyoandaliwa na wafanyikazi wake asubuhi ya leo.

Maandishi ya keki hiyo yalikuwa ‘ siku njema ya kuzaliwa Gushungo’

Gushungo ni jina lake la ukoo.


Sherehe hiyo iiyoandaliwa kwenye ikulu ya rais ilihudhuriwa na majenerali wa kijeshi na wageni wengine mashuhuri walioalikwa.