February 19, 2016

NABII WA MAVAZI ATOKEA JIJINI DAR ES SALAAM.

Magreth - mama anayejitambua kama Nabii, ametokea akidai ana ujumbe aliopewa na Mungu kuwaonya wanawake (hasa wakristo) wasivae nguo zinazoonesha maungo yao bali wavae nguo kama hiyo aliyovaa yeye (pichani kulia). 

Nilikutana na Magreth alipokuja kwenye semina ya uongozi iliyokuwa inahitimishwa leo hapa Mwenge ili aonane na viongozi wa Konferensi na Union awaambie kile Mungu alichomwagiza kwao. 

Hapa anajaribu kujibu maswali kutoka kwa Ndugu Mduma. Magreth ni Mwaadventista anayesali katika kanisa la Kipunguni Ukonga,jijini Dar es salaam na anaonekana kukiamini kwa dhati (conviction) hicho anachokiita mafunuo.

Source: Mtangazaji blog.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.