February 25, 2016

WATOTO WAWILI WAMSHITAKI TB JOSHUA.

Watoto wawili wa Afrika Kusini wanamshitaki muhubiri wa kanisa kubwa na maarufu nchinini Nigeria TB Joshua kwa kifo cha baba yao, wakili wao Bolajii Ayorinde ameiambia BBC.

Wato hao mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na mwingine wa miaka sita wamewasilisha nyaraka za mashtaka katika mahakama ya mji mkuu wa Nigeria, Lagos, wakidai fidia ya zaidi ya dola $521,000; kutoka kanisa la Synagogue Church of All Nations, vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti.

Baba yao alikua miongoni mwa watu 116 waliokufa wakati jengo la makazi yanayomilikiwa na kanisa hilo lilipoporomoka mjini Lagos mwaka 2014.

Mwaka jana mahakama ya uchunguzi wa vifo iliamuru TB Joshua anapaswa kushtakiwa juu ya kuporomoka kwa jengo, akisema kanisa hilo linahusika kwasababu ya uzembe wa kiuhalifu. Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekua wakikana kufanya kosa lolote.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.