March 2, 2016

MHUBIRI ANASWA AKIVUTA COCAINE HUKO UINGEREZA.(+VIDEO)

Muhubiri mmoja wa kikatoliki aliyepatikana katika kanda ya video akivuta kile kilichojulikana kama dawa aina ya Cocaine amechukua likizo ya ukuhani.

Stephen Crossan ameripotiwa kuvuta Cocaine kwa kutumia noti ya pauni 10 katika usiku wa kunywa mnamo mwezi Julai 2015 katika eneo la Banbridge.

Alikuwa katika chumba kimoja chenye kumbukumbu za Nazi na alionekana akisema ''nisingefanya'' huku akivuta,Gazeti la the Sun jumapili liliripoti.
Askofu mkuu wa Dromore alisema katika taarifa kwamba hakuwa na ufahamu kuhusu kisa hicho. Kisa hicho kinadaiwa kutokea katika chumba cha parokia mwezi Julai baada sherehe.

Gazeti la The sun jumapili limedai kuwa kilitendeka katika ile iliojulikana kama nyumba ya parokia ya Crossan katika kanisa la St Patrick Banbridge mwaka 2015.

Tazama video hapa chini.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.