March 22, 2016

VIJANA TUZINGATIE HAYA KUHUSU UTANDAWAZI


VIJANA NA UTANDAWAZI
Kumekuwa na matukio mengi katika mahusiano ya vijana na hata watu wazima ,lakini ningependa kutumia nafasi hii kuzungumzia sana vijana wa rika kama langu(miaka 18-35). 

Katika kipindi cha karibu kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wadogo kujikita katika dibwi la mahusiano katka umri ambao ni mdogo na hiii imepelakea dunia ya maraha kuwa na vita baridi kwa vijana, ambavyo wengi wetu tumekuwa hatumjui adui yetu hasa katika vita hii, nikinukuu kauli ya kiongozi mmoja wa zamani wa jamhuri ya china  alisema  “....hakuna wakati mzuri katika kipindi cha vita kama mwisho wa vita hiyo....““

Katika asiimia 100 ya vijana walio katika mahusiano ya kimapenzi ni kwa asilimia 25 tu ndio kwa hakika wanafuraha ya kweli katika mahusiano yao, kwa mtazamo wangu.

Zifuatavyo ni sababu ya zinatuweka vijana katika wakati mgumu kimahusiano.

  •  Utandawazi
  •  Kutosoma nyakati
  •  Uelewa mdogo wa nini na nani chaguo lako utandawazi

kutokana na ukuaji wa teknologia na sayansi, hali hii imeathiri kwa kiasi kikubwa mahusiano ya vijana katika jamii yetu kwa sasa, vijana wengi tumekuwa ni watu wa kuishi katika jamiii nyingine au tamaduni nyingine katika nyanja ya kimahusiano.,tumekuwa ni watu wa kuiga na kuishi kitamthilia zaidi, na shawishika kusema tunaishi kivenezuela na kifilipino zaidi.

Anyway ni vizuri kujua na kufahamu nini tamaduni na mila za watu wengine , lakini limeibuka tatizo la vijana wengi kutaka kuishi maisha tofauti na tamaduni zetu hilo limepelekea vijana wengi kushindwa kuelewa nini na kwa muda gani vitu hivi vifanyike na kushindwa kuvichukulia vitu kwa ukubwa wake.

Ushauri wangu ni vema vijana tuishi kati yetu wenyewe (yaani katika tamaduni na mazingira yetu)hii itapunguza kwa kiasi kikubwa maumivu na misukosuko miongoni mwetu. Watafsiri wa mambo wanasema ni vema kuishi kama wewe kwani ukishi kama mwingine, hakuna wa kutimiza majukumu yako katika nafasi yako kama wewe ..hivyo ilo litakuwa ni tatizo ambalo mtatuzi ni wewe. So be yourself no matter how is hard to be...
 

Nyakati

Ni kweli mambo yanakwenda yakibadilika na mabadilio kwa binadamu ni kitu ambacho ni vigumu kikizuia, lakini pia sio kila kitu kina badalika au kinaendana na mabadilko hayo, vingine vilikuwepo vipo na vitaendelea kuwepo tu bila kujali kigezo cha muda au Nyakati.


Ni vema tukaliangalia upya swala ili la mabadilko na mahausiano. Kama nilivyosema mwanzo sasa kumekuwa na lundo la vijana wadogo kujiingiza katika mausiano katika umri mdogo, pasipo kuwa na utayari na ukomavu wa akili na kiuchambuzi pia.

Ushauri wangu  ni vema jamii kwa ujumla kukaa na kulizungumzia jambo hili kwa upana na ukubwa wake pasipo kujali rika ili kuweza kukinusuru kizazi hiki cha sasa.  Its better to be open for the best direction

Uelewa mdogo

Hili nitatizo pia kwa upande wake , si tu kujua nini mwenzi wako anapenda na nini hapendi lakini nadhani ni zaidi ya kujamiana,(ngono) mapenzi ni uwanja mpana sana ambao wausika wanahitaji kuwa na uelewa mpana wa kutambua mipaka ya upana huo ili kuweza kuwa na ufanisi mkubwa katika kulitumia jukwaa hilola wapendana nao…

Lakini kuna mengi ya kuyazungumzia na kuchangia pia,nijukumu letu sote kusaidiana na kushauriana pale inapowezekana pia….. kwani kujua bila kufanya siyo kujua(to know without doing is not knowing)By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.