March 31, 2016

MCHUNGAJI APOTEZA WATOTO WANNE KATIKA AJALI YEYE NA MKEWE WASALIMIKA.

Kama kuna jambo limefichwa usoni pa wanadamu ni Kifo, tungelijua sijui tungekuwa na aina gani ya Maisha...
Labda tusingesoma, labda tusingejenga nyumba, labda tusingeoa na kuolewa, labda tusingezaa watoto na yamkini tusingenunua magari wala kusafiri kwa kutumia magari hayo...inabaki kuwa fumbo!
Jana imekuwa siku ngumu na mbaya ambayo itabaki kuwa kovu kwa maisha yote kwa mchungaji Pastory Michael Kajembe ambaye ni mchungaji wa TAG-Ebenezer (Dodoma) Mwanataaluma mahiri wa Theolojia, na Mwalimu wa Chuo cha Biblia Dodoma (Central Bible College, zamani AGBC) na familia yake,Kanisa la TAG kwa ujumla, ndugu jamaa na marafiki...

Baada ya kupata Ajali ya Gari akiwa na familia yake, jana alfajiri katikati ya Mtera na Mpunguzi,Mkoani Dodoma na Kupoteza Watoto wake Wanne kwa pamoja Junior, Isaac, Gabriel na Glady katika ajali hiyo.
Mchungaji Pastory Kajembe na Mama, Bwana amewaponya,bado wanahitaji maombi maana nao wamepatwa na Majeraha na wanaendelea na matibabu.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.