• Isikupite Hii

  March 11, 2016

  APPLE YASHINIKIZWA KUIFUNGUA SIMU MAHAKAMANI

  APPLE

  Utawala nchini Marekani unakata rufaa kupinga uamuzi wa jaji wa kukosa kuamrisha kampuni ya Apple kuifungua simu ya mkononi katika kesi moja inayohusu madawa ya kelevya.

  Wizara ya sheria inatumia sheria sawa na iliyotumia katika majaribio yake ya kwanza ya kuitaka Apple kuifungua simu ya mwanamgambo aliyetekeleza mauaji katika eneo la San Bernardino.

  Serikali ilienda mahakamani baada ya jaji katika neo la Brooklyn kusema kuwa hakuwa na mamlaka ya kutoa amri kama hiyo.

  Katika kesi hiyo, serikali ya Marekani inamtaka jaji kuamrisha Apple iifungue simu ya Jun Feng, ambaye alikiri kuhusika katika ulangusi wa madawa ya kulevya.

  Inataka kutumia simu hiyo kuwanasa baadhi ya washirika wake


  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.