March 20, 2016

Mwimbaji wa gospel atamani kumuoa Lulu wa bongo movie.

Staa wa gospel toka Kenya maarufu kama Bahati amedai kwamba mwigizaji wa kitanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ndiye mwanamke wa ndoto zake.

Akihojiwa kwenye kipindi cha Mseto Bahati amesema kuwa mwigizaji huyo ana sifa zote za kuwa mke wake.

"Nikiweza kupata Lulu, ni kama nitakuwa nimetulia kabisa. Ni kama mtaacha kusikia niko single tena" alisema mwimbaji huyo anayetamba na vibao kama Barua, Itakuwa Sawa na Love.