• Isikupite Hii

  March 1, 2016

  (WEED) BANGI INAVYOHARIBU UBONGO


  Bangi inavyoharibu Ubongo


  Kwa karne nyingi binadamu wamekuwa wakitafuta namna tofauti ili kubadilisha hali yao ya kiakili. Kuanzia kafeini, sigara hadi pombe na madawa ya kulevya.  Lakini namna ambayo hutumika sana (Bangi) ina tofauti gani na madawa na pombe? Na Ina athiri vipi ubongo wa mtu?download

  Kwanza inatubidi tuelewe jinsi ubongo unavyo fanya kazi. Seli za nyuron ndizo zinazo husika na kuchanganua habari katika ubongo na kutuma taarifa sehemu tofauti za mwili kwa kupitisha kemikali maalum kutoka nyuron moja hadi nyingine. Seli hizi hufanya kazi hii kila wakati, unapo waza, unapo kula au kutembea.

  Je, ni kitu gani kinacho endelea kwenye ubongo wa mtu anaye vuta bangi? Tofauti na madawa mengine ambayo yana kemikali tofauti na zile zinazo patikana katika mwili wa mwanadamu, Bangi ina kemikali sawa kabisa na zile zinazo patikana katika mwili wa binadamu (Cannabiniods). Ingawa kwa kawaida Cannabanoids hizi zinapatikana kwa kiwango kidogo kwenye mwili wa binadamu ukilinganisha na zile zinazo ongezwa na uvutaji wa bangi.

  Kawaida seli za ubongo huwa na muda mfupi wa “kupumzika” kila baada ya kupitisha habari kwenda kwenye seli nyingine. Cannabinoid zinapoingia mwilini zina ingilia utaratibu huu kwa kuzuia seli za ubongo (nyuron) zinazo fanya kazi kwa wakati huo kupumzika. Jambo ambalo husababisha nyuron hizo zisambaze habari mwilini kwa kasi sana. Hivyo mtu huendelea kufanya anacho fanya au kuwaza anacho wazo kwa muda mrefu bila kukoma, mpaka pale wazo lingine litakapo mjia mtu.

  Cannabinoid

  Cannabinoid pia huongeza Dopamin, kemikali inayo husika kuleta raha mwilini. Pia zina ingiliamaeneo ya utambuzi, maumivu na njaa katika ubongo, na kusababisha mvutaji kutosikia maumivu, kujisikia furaha na kusikia njaa.   Bangi inavyoharibu UBONGO 
  Je una swali la kisayansi unalo taka kujibiwa? Tuulize kwenye ukurasa wetu wa facebook

  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.