March 8, 2016

Madhara Ya Kunywa Cocacola - Utafiti.

Coca-cola ni nembo kubwa sana katika historia ya nembo ya bidhaa na utafiti umeonyesha ni nembo maarufu duniani baada ya “hallo”, Ni neno la pili maarufu Duniani kwa maana hiyo karibia kila mtu katika sayari hii lazima anywe Coca-cola karibu kila wakati. Jambo hili linatisha kwani imethibitishwa kwamba coca-cola ni hatari kwa mwili wa mwanadamu.
 

Mchanganyiko wa kemikali ambao unakunywa kama kiburudisho kiutendaji inaua umetaboli kutokana na kipimo chake cha uasidi kuwa sawa ni asidi ya betri ya gari.

Sehemu ya tumbo ambapo chakula kinapita kwa ajili ya kuuwa sumu pia inahusisha maradhi kama matatizo ya moyo, kiarusi, pumu, matatizo sugu ya mapafu, nk na ni mbaya zaidi kwa watoto wadogo kwa sababu inaingiliana na mlo bora kuliko kuukamilisha.

Inasemekana kwamba watu wanaokunywa kinywaji hiki chenye sumu wanaangalia utegemezi wa kafeini na upungufu wa madini muhimu kama kalisi, magnesi vitamini A. Usitufikiria vibaya kwani bado tunaamini kwamba

Coca-cola ni kinywaji muhimu ingawaje si kwa ajili ya mwili wa mwanadamu lakini kuna matumizi mengine mengi mazuri ambayo inaweza kutumika na nadhani baada ya kuyajua utaweza kuanza kununua kwa wingi kwa ajili hiyo.

Matumizi 25 halisi ya Coca-cola

Kusafisha Choo: 


Kusafisha choo ni kazi isiyopendeza na hebu tuwe wakweli – hakuna anayependa kuifanya – hakuna yoyote ispokuwa rafiki yake mwenye kufoka Coco-cola. Unachohitajika kufanya ni kumimina kinywaji hicho kwenye karo la choo na usubiri baada ya saa moja alafu uanze kusugua na alafu uvute maji – utakuwa umejipatia choo kisafi chenye kumeremeta.

Madoa doa sugu – Fikiria hapo zamani! Kama hutaki ama huna uwezo wa kununua dawa ya kusafishia madoa au uchafu kutokana na gharama, chukua kinywaji cha Coca-cola na umimine pamoja dawa ya kawaida ya kusafishia au sabuni ya unga. Madoa doa yote yatasafishwa na nguo zako zitakuwa hazina harufu mbaya. Shukran zote ni kwa asidi ya kaboni na ya forforasi ndani ya kinywaji chenye dioksidi ya kaboni.

Kusafisha vioo vya Madirisha: 


Mpaka sasa tumeweza kufahamu maajabu ya nguvu ya kusafisha ya Coca-cola – Kitu kingine ambacho kinaweza kusafisha vizuri ni vioo vya madirisha. Kutokana na asidi ya sitriki inayopatikana katika kinywaji hicho, kinasababisha kun’garisha vioo na inafanyakazi kama linavyofanya kazi tunda la sitriki katika kazi kama hiyo.

Kuuwa Wadudu: 


Wadudu wengi ni wapenzi wa Coca-cola ina maana hata sisi wenyewe, wanapenda utamu na ufokaji wa kinywaji hicho lakini hatujui/hawajui kama kinaweza kuhatarisha afya au maisha yao na badala yake tunandelea kukinywa. Unaweza kunyunyiza kinywaji hiki katika kichuguu au kabatini kwako na kuwaangamiza kabisa mchwa na mende waliokusumbua.

Kukoleza Rangi inayofifia:


Unaweza kutumia kinywaji hiki katika nywele zako kama ulitia rangi nywele zako na zimekolea sana. Coca-cola inafahamika kwa ubora wake wa kufifiza rangi kwenye nywele, kwa maana hiyo kama ulipaka rangi katika nywele kwa namna ambayo uiridhii usishtuke kwa kumwendee msusi mwenye gharama bali fungua fridge yako na utoe kinywaji cha Coca-cola na kitakufanyia kazi nzuri.

Kuondoa Gundi: Kama gundi imen’gan’gania katika nywele zako na unafikiria kwamba njia pekee ya kuiondoa ni kuzinyoa nywele zako basi usipata tabu tena! Kitu cha kufanya ni nyunyiza kinywaji cha Coca-cola katika sehemu iliyopo hiyo gundi na usubiri baada ya dakika chache na utaona kwamba itakuwa rahisi kuiondoa hiyo gundi bila tabu kutoka kwenye nywele zako.

Kuondoa maumivu: Kama umeumwa na mdudu, nyuki, au kiwavi basi usipate hofu, mimina kinywaji cha kufoka foka katika eneo lililoathirika na maumivu yataondoka baada ya sekunde chache, shukrani kwa kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha Coca-cola.

Kuosha vyombo: Kama vyombo vyako vimekuwa vyeusi, mimina kinywaji cha miujiza katika vyombo hivyo na uiache kwa dakika chache. Kemikali zilizopo katika kinywaji hicho kitaondoa uchafu uliopo na baadae unachohitaji ni kusugua na vyombo vyako vitakua safi na vyenye kun’gara.

Kiondoa kutu: Kama unataka kuondoa kutu, tumbukiza kitu kilichokuwa na kutu katika chombo ulichomimina kinywaji cha Coke au kama kitu hicho si kikubwa basi lowesha kipande cha nguo ndani ya coke alafu ufute kila kitu kilichokuwa na kutu. Asidi ya fosforasi iliyopo kwenye kinywaji hicho kitalainisha kutu iliyopo kwenye kitu hicho na kuiondoa kabisa.

Kuuwa Wadudu Shambani: Huko India baadhi ya wakulima hutumia Coca-cola badala ya dawa za kuuwa wadudu kufanya kazi hiyo, kwa sababu ni rahisi na ufanisi na matokeo yake ni mazuri zaidi. Inasemekana kwamba kiwango cha juu cha sukari kinachopatikana kwenye kinwyaji hicho kinazidisha ubora wa kupambana na wadudu, kitu ambacho kimekanushwa na kampuni hiyo kwani wamesema kwamba hakuna chochote katika kinywaji hicho ambacho kinawezesha uuaji wa wadudu. Lakini mbinu hizo za kupinga zinaonekana kama ni janja ya nyani kwa wakulima wa huko India.

Kiyeyusha Barafu: Coca-cola inaweza kuyayusha barafu ambayo huganda kwenye vioo vya magari wakati wa kipindi cha majira ya baridi. Nyunyiza kinywaji hicho katika sehemu ambayo barafu imeganda na iwacha ikolea kwa dakika chache na hatimae barafu itayayuka.

Kuwatega Wadudu: Kama kunapatikana wadudu wengi kwenye eneo au kwenye bustani yako na inakuwia vigumu kuwaua mmoja mmoja basi weka makopo ya kinywaji cha Coca-cola katika maeneo ya bustani yako au karibu na dirisha na wadudu hao watavutiwa na kujikusanya katika makopo na hivyo kukurahisishia kuwaua kirahisi.

Kuondoa Harufu mbaya: Hauna haja ya kukabiliana na harufu mbaya tena. Kama umepita sehemu na kwa bahati mbaya ukanyewa na dege au mnyama yoyote na unalazimika kuondoa harufu hiyo mbaya basi si lazima kukimbilia kujipulizia au kujipaka mafuta mazuri. Kitu cha kufanya ingia bafuni na ujimwagia kidogo kinywaji hicho katika eneo iliyodhurika na baada ya kujimwagia maji harufu hiyo itakuwa imeondoka.

Msaada katika bustani yako ya majani: Pia huu ni msaada wa mara moja katika bustani yako ya majani. Kama utamwagia kopo moja la coke kila wiki katika vilindo ulivyoviweka katika sehemu mbali mbali za bustani yako ya majani, itasaidia ukuaji wa vidubuni ambayo baadae vitasaidia kunawirisha bustani yako ya majani na kufanya ikuwe vizuri.

Kusafisha Sarafu: Kama wewe ni mkusanyaji wa sarafu basi bila shaka utapenda kidokezi hiki, unaweka kuingiza sarafu zako katika chombo iwe ni glasi au bakuli lililojaa kinywaji cha Coca-cola na uziwacha kwa muda kidogo. Ukitoa baada ya muda utashangaa kwa kuona sarafu zako zikin’gaa na zikiwa kama mpya tena. Cola inasaidia kuondoa samadi au uchafi uliojikusanya.

Kusafisha uchafu vichwa vya betri: Asidi inayopatikana katika kinywaji hiki ni ndogo kiasi ukilinganisha na ile ya kawaida ambayo ikimwaga kwenye betri haiwezi kufifilisha asidi ya betri (H2SO4), ambayo ni asidi haswa, na hii inammainisha inaweza kutumiwa kusafisha betri zilizochafuka. Kwa maana hiyo kama umekwama porini na unahitajika kusafisha betri yako na

hauna cha kusafishia isipokuwa una Coca-cola (tutashangaa kama utashindwa kukichukua kinywaji hiki ukiwa safarini baada ya kusoma makala hii) unaweza kukitumia kwa ajili ya kusafishia.
Kitu cha kulegeza: Unaweza kutumia kinywaji cha Coke kulegeza bolti zilizokaza na zilizoshika kutu. Nyunyiza kinywaji hicho kwenye sehemu hiyo ya bolti na uiwache kwa muda kidogo na baadae unyunyiza maji kidogo alafu uifungue na utagundua imelegea kiasi.

Baada ya kufahamu maajabu ya kuhusu kinywaji cha Coca-cola tunajua unajuta kukitumia na kuhatarisha maisha yako kwa kunywa sumu hiyo kidogo kidogo. Lakini kwa sababu sasa unafahamu kwa hivyo mara nyingine ukiwa katika tafrija ambayo unalazimika kuhudumia kwa sababu

kutainusuru familia yako na wewe mwenyewe na madhara yatokanayo na unywaji wa Coke, kusanya mabaki yote ya kinywaji hiki na umimina katika chombo kimoja kikubwa kwa ajili ya kusafisha uchafu na kutu inayopatikana katika vyombo ili vin’gara.
 


By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.