March 3, 2016

POLISI WAMKAMATA MKURUGENZI WA FACEBOOK NCHINI BRAZIL.

Mkurugenzi mkuu wa Facebook nchini Brazil amekamatwa na maafisa wa polisi baada ya kampuni hiyo kukataa kufuata maagizo ya mahakama katika kesi moja ya mihadarati,maafisa wa polisi wamesema.

Kulingana na ripoti, makamu wa rais wa Facebook wa eneo la Marekani Kusini,Diego Dzodan alikamatwa na kuhojiwa katika mji wa Sao Paulo siku ya Jumanne.

Maafisa wa mahakama katika jimbo la Sergipe walitoa agizo hilo akamatwe.Facebook imesema ni makosa makubwa.
Facebook imekuwa na itakuwa ikijibu maswali yoyote kwa serikali ya Brazil,kampuni hiyo ilisema.

Imeongezea kuwa hatua hiyo inahusisha huduma ya WhatsApp ambayo inafanya oparesheni zake tofauti na facebook.

Polisi wa kijimbo mjini Sao Paulo wamesema kuwa walitekeleza agizo la mahakama la kumkamata afisa huyo lililotolewa na jaji wa kesi za uhalifu wilayani legarto katika kijimbo kidogo cha Brazil cha Sergipe.

Taarifa iliotolewa na polisi imesema kuwa facebook iliagizwa kutoa ushahidi ambao utasaidia uchuguzi dhidi ya uhalifu wa kupangwa pamoja na ulanguzi wa mihadarati ambao umekuwa ukifanyika katika faragha.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.