March 8, 2016

MILLARD AYO AWATIA MOYO WANAFUNZI WALIOFELI KIDATO CHA NNE.

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Millard Ayo baada ya kufungua studio yake kubwa naya kisasa jijini Dar, ameanza kuuza vipindi vya burudani katika radio mbalimbali za Afrika Mashariki.


Akizungumza Jumamosi hii katika mdahalo wa kuwatia moyo wanafunzi waliofeli kidato cha nne, ambao ulienda sambamba na uzinduzi wa video mpya ya Mrisho Mpoto, Millard alieleza mafanikio yake baada ya kupambana kwa muda mrefu.

“Nilijiuliza kwanini nisitumie uandishi wangu wa habari ili kusambaza habari Afrika?, ndipo nikaanza kujinyima ili nijenge studio yangu kwa pesa yangu mpaka imekamilika. Sasa hivi tayari nimeshaanza kuuza vipindi vyangu katika radio mbalimbali za Afrika, Kenya, Rwanda. 

Pia nimekuwa reporter wa radio mbalimbali za Afrika Mashariki, pia Nigeria kuna kazi maalum nimepata ambayo nimehifurahia sana,” alisema Millard.

Pia Millard Ayo alisema yeye ni miongoni mwa wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne lakini aliinuka na kuendelea.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.