March 29, 2016

MUZIKI WA GOSPEL TANZANIA NANI AMEULOGA?

Kupitia  ukurasa wake facebook Mwanaharakati Martin Bashando aliyasema maneno haya.

"Muziki wa Injili Tanzania umeanza miaka mingi sana zaidi ya Bongo fleva, lakini sijawahi kuona record ya mwanamuziki wa injili ambae amewahi kufanikiwa kifedha pamoja na kuufikisha muziki wake katika viwango ambavyo huyu mwanamuziki Diamond ameufikisha mziki wake. 

Wanamuziki wengi wa Injili wa hapo zamani walipofanikiwa katika muziki wao kidogo wengi walikimbia na kuhamia ulaya, na walipofika kule kasi ya muziki ilipungua kwao na kujikuta wanakimbizana na maisha kwa kufanya vibarua vya kufyeka garden za wazungu, kufua, kuosha sufuria, kuogesha farasi, kutunza wazee nakadharika, lakini pamoja na kuwa waliendelea na fani zao Polepole lakini hawakuweza kusimamia kipaji hadi kufikia viwango vya kuipeperusha bendera ya nchi katika viwango hivi vya Diamond.

Kwa miaka ya 2000 hadi 2015 ndipo walichipuka wanamuziki wa Injili ambao angarau walijitahidi kidogo sana katika fani zao huku wakiwa hapa hapa nyumbani na wakashika vijimilioni na kumiliki magari pamoja na kujenga nyumba na wengine kuwa na biashara pembeni, lakini bado hawajafikia kiwango cha kuwa wanamuziki wa kimataifa bali wanakuwa wanamuziki wa afrika mashariki.

Katika mchakamchaka huo anaetuokoa kidogo ni Rose Muhando ingawa juhudi zake zinapuuzwa na watu wengi wanampiga vita vikali sana kupitia mapungufu yake ya kibinadamu.

Sasa najiuliza hapa tofauti iko wapi ama tatizo liko wapi hadi waimbaji wa nyimbo za Injili wanaishia katika kiwango kidogo na wanashindwa kupenya na kufikia levo kubwa ambazo wanastahili na kujikuta kila siku wako pale pale ingawa kiuharisia wana vipaji vikubwa sana zaidi ya bongo fleva?"

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.