• Isikupite Hii

  March 22, 2016

  BAADA YA KUKEMEA USHOGA, APIGWA MARUFUKU KUINGIA KWENYE MALL MAARUFU MAREKENI.

  Baada ya kampuni ya Nike kusitisha mkataba na bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao kufuatia kauli yake kuwa mashoga ni wabaya zaidi ya wanyama, mall maarufu ya jijini Los Angeles, Marekani, Grove imempiga marukufu.
  Manny Pacquiao
  Mmiliki wa mall hiyo, Rick Caruso amedai kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwakuwa watu wengi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni wateja wa mara kwa mara wa mall hiyo na kwamba wana haki ya kujisikia vibaya.

  “Hivyo Manny Pacquiao hakaribishwi tena,” alisema.

  Kauli hiyo iliyowakasilisha watu wengi wanaojihusisha na mapenzi hayo ilimfanya aombe radhi.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.