March 30, 2016

RAILA ODINGA AANGUKA JUKWAANI ALIPOKUWA AKISIMULIA KUHUSU MATESO ALIYOPITIA YESU KRISTO. (+VIDEO)

Video inayoonesha kiongozi wa upinzani Kenya Bw Raila Odinga na viongozi wengine wakianguka baada ya jukwaa kuporomoka akihutubia mkutano wa hadhara imevuma sana mtandaoni Kenya.

Bw Odinga alikuwa akihutubu katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Malindi, jimbo la Kilifi katika pwani ya Kenya Alhamisi wiki iliyopita jukwaa lilipodondoka.

Mkutano huo ulikuwa wa kuwashukuru wapiga kura kwa kumpigia kura mgombea wa chama chake cha ODM Willy Mtengo kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Machi 7.

Ilikuwa siku moja kabla ya Ijumaa Kuu na Bw Odinga alikuwa akisimulia kuhusu mateso aliyopitia Yesu Kristo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.