March 22, 2016

PAPA FRANCIS AJIUNGA NA MTANDAO INSTAGRAM.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amejiunga na mtandao wa kijamii wa Instagram.

Papa Francis alijiunga na mtandao huo unaotumiwa kupakia na kusambaza picha Jumamosi.

Saa moja pekee baadaye alikuwa amepata wafuasi 10,000.
Anajiita @Franciscus, ambalo ni jina Francis kwa Kilatino.
Amepakia picha tatu kufikia sasa na wafuasi wake walifika 1.5 milioni kufikia Jumatatu lakini hajamfuata yeyote.

Picha yake ya kwanza kupakia kwenye Instagram inamuonyesha yeye akiwa amepiga magoti na kuinamisha kichwa akiomba na kuandika: “Niombeeni”.

Papa Francis amekuwa kwenye Twitter ambapo hujiita @Pontifex na aliitumia kutangaza kwamba ameingia kwenye Instagram. Kwenye Twitter, ana wafuasi 8.9 milioni.

Papa Francis huongoza waumini karibu 1.2 bilioni wa Kanisa Katoliki la Kirumi kote duniani.

Akaunti hiyo yake ya Ingtagram itasimamiwa na watu wengine Vatican.

Inaaminika kanisa hilo linajaribu kuwasiliana zaidi na vijana kwa kutumia mitandao ya kijamii.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.