March 31, 2016

RACHEL KIZUNGUZUNGU AMRUDIA MUNGU, MUZIKI WAKE JE? (SOMA HAPA +VIDEO)

Mwimbaji Rachel ambaye ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kujiunga na nyumba ya vipaji Tanzania (THT) na kuanza kuachia nyimbo zake, amekaa kwenye Excluvie na mtangazaji wa Amplifaya ya CloudsFM Millard Ayo na kueleza kilichotokea mpaka akakwama na kukaa kwenye nchi ya watu kwa zaidi ya miezi saba, ishu yake ya kuvuta bangi na kumrudia Mungu.

"Ni kweli nimemrudia Mungu, ni maamuzi ambayo nimeyafanya mwenyewe baada ya kuona vitu ni vilevile, dunia ni ileile na watu ni walewale ndio maana nikaona sio vibaya nikaja na upande mwingine lakini hii haimaanishi kwamba nitakua nafanya muziki wa Injini, nitaendelea na bongofleva lakini muda mwingi nitautumia kanisani." alisema Rachel

Kuhusu bangi na madawa ya kulevya check video hapa chini.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.