May 1, 2016

Wachungaji 2 na muumini 1 wafariki katika ajali ya gari.

Wachungaji wawili wa kanisa la FPCT, na mshirika mmoja wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya gali eneo la Mabama wilayani Uyui walipokuwa wakisafiri kutoka Mishamo wilayani Mpanda mkoani Katavi, wakielekea jijini Mwanza katika mazishi ya mchungaji wao kiongozi.

Akiongea na kituo cha ITV katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete, mchungaji Banyiyezako Serestini, majeruhi, amewataja marehemu kwa majina ya mchungaji Ndezimana Sefania, na mchungaji Pili Simion, na mshirika ambaye hakufanikiwa kumkumbuka jina mara moja ambaye amefariki hakiwa hospitalini.

Soma: Mchungaji Apoteza Watoto Wanne Katika Ajali Yeye Na Mkewe Wasalimika.

Aidha akiongea kwa masikitiko askofu wa jimbo la Tabora Mhashamu Issaya Ilumba amewataka madreva kuwa waangalifu wanapokuwa wanawaendesha viongozi mbalimbali na si kanisa hilo bali taifa zima kuwa waangalifu kuepusha ajali. 

Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa na nusu 21/04, baada ya gurudumu la mbele kushoto, la gali aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili TNA kupinduka mara mbili na kusababisha vifo viwili papo hapo na mmoja katika hospitali ya rufaa ya Kitete Tabora.