April 7, 2016

CHRISTINA SHUSHO APATA DILI KALI AFRICA MAGIC (DSTV).

Star wa muziki wa Gospel Tanzania Christina Shusho amepata dili mpya ya kua Mtangazaji wa Kipindi Kipya kitakacho rushwa na Chanel Ya Africa Magic Bongo DStv Channe 160. Kipindi hicho kilicholenga kutoa support ya muziki wa Gospel Tanzania hususani kulenga waimbaji wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa Gospel.

Tarehe 4/4/2016 Timu ya Africa Magic ikiongozwa na Director mkongwe Jblessing ilipiga kambi Tanzania na kufanya Interview na baadhi ya waimbaji wa Gospel pamoja na watangazaji wa vipindi vya Gospel kutokea hapa nyumbani Tz. Kama kawaida Timu Ya Chomoza Ya Clouds TV ilipata nafasi ya kuchambua/Kutoa picha halisi ya muziki wa Gospel toka ulipo anza na unapo kwenda. Niwazi kabisa kumekua na mabadiliko makubwa katika muziki wa Gospel tofauti na miaka 10 iliyokwisha pita hasa katika utayarishaji wa Audio na Video alisikika Uncle Jimmy akieleza.
Jblessing
Kupatikana kwa dili hii mpya ya Christina Shusho kuwakilisha muziki wetu wa Gospel Africa Magic kutatoa nafasi kubwa kwa waimbaji wetu kujitangaza vizuri Duniani. Africa Magic ni kituo kikubwa barani Africa na uonekana sehemu kubwa duniani kupitia DStv….hii ni nafasi nzuri kwa waimbaji wetu wa Gospel kujipanga vizuri kuanzia Audio pamoja na video kwakua dunia itakua ikiwamulika.

Soma: Gospo singer ataka kufanya collabo na diamond platnumz

Kwa sasa Christina Shusho atakua akifanya kazi Kenya na Tanzania akihoji waimbaji tofauti tofauti wa muziki wa Gospel. Kutokana na kua na kazi mbili za kufanya Tanzania na Kenya Christina Shusho aliamua kujenga Studio ya kisasa huko Segerea ambako ndiko kutakapokua kukifanyika kazi za recording pamoja na video production ya vipindi vyake.
 Christina Shusho Na Uncle Jimmy 
Kupatikana kwa shavu hilo kwa mwana Mama Christina Shusho kumemuongezea thamani kubwa ya muziki wake pamoja na mashabiki wapya watakao kwenda kuona kazi zake Duniani kupitia DStv. Mungu ibariki Tanzania Mungu bariki muziki wetu wa Gospel TZ.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.