April 9, 2016

DARAJA LA KUUNGANISHA BARA LA AFRIKA NA ASIA KUJENGWA JUU YA BAHARI YA SHAMU.

Mfalme wa saudia ametangaza kwamba daraja linalounganisha taifa hilo na Misri litajengwa juu ya bahari ya shamu.


Mfalme Salman alisema katika taarifa kwamba daraja hilo litaimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.

Alitoa tanagazo hilo wakati wa siku ya pili ya ziara yake katika mji mkuu wa Cairo.Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alisema kuwa daraja hilo litatajwa baada ya mfalme huyo wa saudia.

Soma: Ndege kubwa na yenye uwezo wa ajabu duniani

Rais Sisi ni mshirika wa karibu wa serikali ya Saudia.

“Tulikubaliana na ndugu yangu rais Abdul-Fattah al-Sisi tujenge daraja linalounganisha mataifa yetu mawili”, alisema mfalme huyo.

“Hii ni hatua ya kihistoria ya kuunganisha mabara ya Africa na Asia na itaimarisha biashara kati ya mabara haya mawili”, aliongezea.

By Chief Hope 


Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.