April 28, 2016

MTOTO WA MIAKA 2 AMUUA MAMAKE MAREKANI.

Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa katika mji wa Milwaukee, Marekani.
Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari.

Mwanamke huyo, Patrice Price, 26, alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye ni mlinzi na ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari, babake Andre Price amesema.

Soma: Visa Vya Kujiua Vimeongezeka Canada

Polisi wa Milwaukee wanasema mwanamke huyo alipigwa risasi moja kutoka nyuma akiendesha gari mapema Jumanne asubuhi.

Mwezi uliopita, mvulana wa umri wa miaka minne alimpiga risasi mamake Jamie Gilt katika jimbo la Florida katika hali sawa. Bi Gilt alinusurika na majeraha.

Source: Bbc Swahili.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.