April 28, 2016

CHRISTINA SHUSHO NA JOHN LISU WAINGIA KATIKA TUZO ZA GROOVE. (KENYA)

Mwanamuziki nguli wa muziki wa injili Tanzania hasa kwa upande wa kuchukua tuzo za kimataifa Christina Shusho ameweza kuingia tena kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Groove za huko nchini kenya katika kipengele cha Eastern and Central Africa Artist of the year (Msanii bora wa mwaka kutoka Afrika mashariki na kati) safari hii akiwa pamoja na mtaalamu wa muziki wa Live John Lisu ambaye yupo katika kingele hicho.

kwa upande wa shusho sio mgeni kwenye tuzo hizo kwani ameshawahi kushiriki huko nyuma na kufanikiwa kuchukua kadhaa tofauti na John Lisu ambaye pengine inaweza ikawa ndio tuzo yake ya kwanza kushiriki. 

Download Wimbo: Waranda Randa Mbao - Christina Shusho.

Shusho na Lisu wanashindana waimbaji wengine kama Alarm ministries (Rwanda), Bugembe Wilson (Uganda), Coopy Bly (Uganda) na Rebecca Soki (DRC).

Groove wameshatoa mchakato wa kupiga kura na tayari wameshafungua mchakato huo ambao unafanyika kupitia tovuti yao ambayo ni www.grooveawards.co.ke kisha unaenda sehemu iliyoandikwa vote now.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.