April 19, 2016

MUNGU AZIDI KUMUINUA UPENDO JBRIDE HUKO CANADA.

Upendo JBride Mwakyengula ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania. Mungu amemtoa mbali sana katika huduma yake ya uimbaji, na amepitia mapito mengi mpaka hapa alipo. 

Kinachomsaidia mwimbaji huyu katika mapito yote ni imani yake aliyoiweka kwa Mungu. Mwimbaji huyu ni mwimbaji jasiri na mwenye kujiamini na kuamini kile anachokiimba, watu wengi wanabarikiwa na wengine kuokoka/kupokea uponyaji kupitia nyimbo zake.  

Soma: Picha Za Ghorofa (Jumba Jipya) La Askofu Dastan Maboya.

Mungu anamtumia kwa namna ya kipekee sana na ndio maana amekuwa akipokea mialiko mbalimbali mara nyingi ya kwenda kuhudumu nchi za Ulaya, Canada na Marekani. Kama Watanzania hatuna budi kumsapoti na kumuombea mwimbaji huyu kwa sababu amekuwa balozi mzuri wa kupeperusha bendera ya Tanzania katika mataifa mbalimbali Duniani kote.

Upendo alisema haya kupitia account yake ya Facebook "For all who prayed for me may the Lord bless you. We had a powerful African Revival Conference here in Edmonton Canada. Thank you Pastor Leonard & Lorie Rutten of Enjoy Life Church , Pastor Boniface and Happy Mgonja, Pastor Zephania & Ruth Ryoba, Mr.Tumaini & Rachel Mhehe ..and all , God bless you. To God be the Glory for all He has done in Canada.‪#‎MissionAccomplished‬." 
Baadhi ya picha za Upendo Jbride akihudumu huko Edmonton Canada.
By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.