April 1, 2016

ALIYEWAKINGA WAKRISTO KUTOKA KWA AL SHABAB ATUZWA.

Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.
Mwalimu Farah

Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.

Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.