May 6, 2016

MUME WA MWANAMUZIKI HUYU WA INJILI APATA AJALI YA PIKIPIKI.

Mume wa mwanamuziki wa injili Tanzania Angel Benard, Bw.Godsave Sakafu kupitia akaunti yake ya facebook ametoa taarifa kuwa siku ya leo (juzi) amepata ajali ya pikipiki ambayo alikuwa akiiendesha.

Soma: Angel Benard Ajifungua Mtoto Wa Kiume.

Godsave ameweka picha yake inayoomwonesha akiwa na majeraha sehemu za usoni na kichwani na kuandika maneno yafuatayo akielezea ajali hiyo..
"Namshukuru Mungu leo tarehe 5 ameniepusha na mauti. Nimepata ajali mbaya ya pikipiki ambayo nilikuwa nikiiendesha mwenyewe ambapo nikiwa barabarani mvua ya upepo ilianza kunyesha na hivyo nikashindwa kuona vizuri na katika harakati za kutoka main road ndipo tairi ikatereza na pikipiki ika gonga kalavati na kunitupa nga’mbo ya mtaro na pikipiki kutumbukia mtaroni.Nilipoteza fahamu na baada ya fahamu kurudi nilikuwa njiani kwenda hospitali na nimepata majeraha kichwani na usoni na meno mawili yamevunjika ila namshukuru Mungu nimetoka salamaKesho ilikuwa niwe mnenaji katika mkesha pale pabtist church na bado nitaenda pamoja na yote"
Source: Gospomedia.com

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.