May 19, 2016

BONDIA MAARUFU DUNIANI KUTUMIA ZAIDI YA TSH BILIONI 14 KUJENGA KANISA.

Bondia maarufu duniani Manny Pacquiao na Mbunge wa jimbo la Saragani nchini Ufilipino ameweka bayana mikakati yake ya kujenga Kanisa

Pacquao amesema kanisa analolijenga nchini Ufilipino litagharimu kiasi cha dola za kimarekani $6.7Millioni ambazo ni sawa na zaidi ya hela ya kitanzania Bilioni 14. Kwa mujibu wake ujenzi huu ni sehemu ya yeye kumshukuru Mungu kwa yale alotenda maishani mwake.

Soma: Siri Za Matajiri Wakubwa Zafichuka.

Akiongea na mtandao wa Philboxing, Pacquao amesema kanisa hilo litajengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa Hekta Mbili ambapo ndani yake kutakuwa na Chuo cha Biblia, makazi ya Mchungaji, ofisi na sehemu maalumu ya kusomea Biblia.
Mradi huu unakadiriwa utachukua miezi takribani 18 ili kukamilika. Ujenzi wa kanisa hilo ulizinduliwa na mmoja wa maaskofu nchini humo ambaye amekuwa akimfahamu bondia huyo kwa muda mrefu.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.