May 13, 2016

Mwigizaji 'Kajala Masanja' aamua kuokoka na kumrudia mungu.

Siku chache zilizopita, mwigizaji wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja alitangaza rasmi kuwa ameokoka na hivyo ameamua kumrudia Mungu kwa sababu ameona mambo ya kidunia kwa wakati huu hayana nafasi na si ya kuyaendekeza.

Soma: Yna Wa The Promise Ajikita Kumcha Mungu Na Kulea Familia Yake, Aweka Pembeni Uigizaji.

Akizungumza Kajala alisema kwa sasa ameamua kuabudu kwenye kanisa moja la kiroho lililopo Kibamba jijini Dar na kukiri kuwa tangu ajiunge huko, amekuwa akifunguliwa mambo yake mengi ikiwa ni pamoja na kujitambua.
“Nimeamua kwa akili yangu mwenyewe kurudi kwa Muumba wangu kwa sababu haya mambo ya kidunia yana mwisho wake na hata mastaa wenzangu wanapaswa kumuabudu Mungu hata kwa juma mara moja kwa maana chochote walicho nacho ni kwa ajili ya yeye,” alisema Kajala.