May 11, 2016

Mchungaji ajifunga minyororo kumtaka rais aachie madaraka.

Mchungaji mmoja huko nchini Zimbabwe ajulikanaye kwa jina la Patrick Philip Mugadza ambaye mapema mwezi disemba mwaka jana aliandamana peke yake akipinga utawala wa Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo. 

Safari hii ameamua kujifunga mnyororo huku akiwa ameshikilia msalaba mkono mmoja na mwingine Biblia kabla hajaanza kuzungumza na wapita njia kwa muda wa lisaa moja na nusu akiwa na mada isemayo "Nini tunatakiwa tukifanye ili tuwe huru kutoka katika matatizo yanayowakabili taifa lao". 

Mchungaji huyo anayechunga kanisa la Remnant alifunguka kwa kuwaambia wapita njia kuacha woga wa kijinga kwa kukaa kimya wakati wanajua fika kwamba nchi yao ipo kwenye mwelekeo mbaya huku wakitazama.
Amesema "kuna haja ya uhuru sio uhuru wa nchi tu bali uhuru katika mambo mengi ya msingi kama utekwaji, kupigwa na kufungwa midomo kwa waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu kwaajili ya kusema ukweli bado kuna watu wanasema tuna uhuru, mpaka pale tutakaposimama na kusema vinginevyo hakutakuwa na mabadiliko katika nchi yetu. Wazimbabwe tunahitaji kudai uhuru wetu, mafanikio na kazi" alisema mchungaji Mugadza
Mpaka tutakapoandamana na kusimama mitaani kudai uhuru wetu, tutazidi kuona taifa letu linanyonywa hadi umauti, viwanda vimebadilishwa na kuwa vyo vikuu, ikimaanisha hakuna maono ya viwanda tena nchini alisema mchungaji huyo. 

Aidha mchungaji huyo alitumia andiko kutoka kitabu cha Yeremia 29:11 kama maombi yake kwamba Mungu awaguse watu wote wanaoliongoza taifa hilo kuungana nao katika mateso wanayoyapata na kuliinua taifa lao tena.

Source: GospelKitaa.


Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.