May 12, 2016

Ukifanya haya kwa mume wako, ndoa yenu itadumu milele.

1. Muite kwa jina lake la utani.

2. Muache atumie mamlaka yake kama kichwa cha nyumba.

3. Usimcheke akiwa ameumizwa na jambo fulani.

4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira
Unaweza ukaenda kumuomba msamaha na kumueleza kwanini ulimkosea pale hasira zinapokua zimemuisha.

5. Kuwa na haraka ya kuomba msamaha pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe.

6. Ongelea mazuri yake na yeye kabla ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya hivyo.

7. Waheshimu wazazi wake.

Soma: Mambo Matano Yanayodhoofisha Mahusiano Na Ndoa

8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kuwapelekea chochote. Na afanye hivyo na kwa wazazi wako pia.

9. Msuprise kwa chakula akipendacho, hasa kipindi kile anapokuwa na msongo wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.

10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumie chakula mume wako ukiwa nyumbani.

11. Mkaribishe kwa kumkumbatia anapotoka kwenye mihangaiko yake. Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.

12. Tabasamu pale unapomtizama, vaa vizuri na jipendezeshe pale mnapotoka wote kwenda kwenye warsha mbalimbali.

13. Mpigie simu na umwambie kwamba unampenda na umemkumbuka.

14. Muamshe asubuhi na umpe romance kiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpe na hata jishughulisha na wanawake wengine siku hiyo.

15. Kamwe usithubutu kutamka kuwa hakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.
16. Mwambie ni kiasi gani una bahati kuwa nae kama mume wako.

17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.

18. Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamu wako katika maisha yako.

Soma: Sifa 7 Za Mwanamke Wa Kuoa (Wife Material).

19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhi mikononi mwa Mungu.

20. Tengenezeni utaratibu wa familia nzima kumshukuru Mungu kwa pamoja  kila asubuhi na usiku kabla ya kulala.

Mungu abariki ndoa yako. Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya kweli leo na daimaNa wasio serious na mahusiano wanaokupotezea muda wako wajikatae kwako mapema ili wasikuzibie nafasi ya kutimiza kusudi la Mungu kwako.

Kwanini tusiseme "Amen"!?