May 9, 2016

VIDEO YA RINGTONE NA CHRISTINA SHUSHO IMEMGHARIMU ZAIDI TSH. MILLION 21.

Alex Nyanchoga Apoko "Ringtone" ni mwanamuziki wa injili nchini Kenya ambaye amedumu Kwenye Industry kwa muda mrefu na amewahi kuonyesha nia ya kuwania ubunge katika jimbo moja nchini Humo.

Tazama Video: Tenda Wema - Ringtone Ft Christina Shusho.

Hivi karibuni Ringtone amekuja na video ya nyimbo iitwayo TENDA WEMA ambayo amemshirikisha Christina Shusho
Akiongea na mtandao wa SDE Ringtone amesema nyimbo yake na Shusho imemgharimu 1Million Kenyan Sh ambayo kwa exchange rate ya leo 9.5.2016, 1Ksh=21.81Tsh hivyo basi kibongo bongo Ringtone ametumia zaidi ya shilingi 21Million kwa video moja.

Ringtone amezidi kusema sababu kubwa zilizopelekea video hiyo kufikia kiwango hicho ni pamoja na kukodisha ndege mbili(Chopa/Helicopter) zilizomgharimu kiasi cha Ksh 500,000/= sawa na zaidi ya 10M ya kitanzania pamoja na mambo mengine mengi alitumia zaidi ya 21M Tsh.
Tukirudi nyumbani Tanzania gharama za Ringtone kufanya nyimbo moja kwa bei hiyo ni funzo tosha kwa Musicians wa Tanzania wanaotegemea chieap Video

Soma: Victor Mbagga Kuachia Dvd Album (Mpya) Hivi Karibuni.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.