May 25, 2016

Ajitosa katikati ya simba akidai kaagizwa na Mungu.

Siku ya tukio nchini Chile, kijana Franco Luis Ferada Roman aliamua kutembelea eneo lililohifadhiwa wanyama, (Zoo) , na kulipia kiingilio kama watu wengine waliojitokeza. 

Lakini ndani yake, akili ilikwishaamua, ya kwamba ni lazima aingie ndani akakutane na simba, na wala hakutaka simba wahangaike kuzichambua nguo kabla ya kumtana, alimua kuweza nguo zake kando na kisha akatumia njia ya paa kuingia ndani ya boma hilo la simba
Kwa maelezo ya kijana Franco anadai kwamba amesikia sauti ikimtuma kuingia humo ndani ya uzio wa simba. Kufanya nini? Hajaeleza zaidi, lakini tarehe 21 Mei ndio siku aliyochagua kufa. Japo haikuwezekana.
Taharuki ilianzia papohapo kwa watazamaji waliotembelea eneo hilo, kuona kijana akiwa kando ya simba kama alivyozaliwa, na kisha wale simba wakaanza kumzonga zonga, lakini wakicheza naye kwanza. 
Kelele za nje na pengine hofu iliyotibuliwa ndiyo ilipelekea simba nao kumaliza mchezo wao baada ya kushindwa kujua nia ya Franco ni nini, na hivyo kuanza kumpelekesha, jambo lililofanya Franco aanze kupiga kelele na kulitaja jina la Yesu

Soma: Wachungaji 10 Matajiri Zaidi Duniani (Hawa Hapa). 

Isingekuwa kwa walinzi wa eneo hilo ambao walilazimika kuwaua simba wawili kati ya watatu waliokuwemo humo ndani kwa risasi, basi huenda Franco angeshakuwa amechongewa jeneza sawasawa na urefu wake. 

Madaktari wanaomtibu wameeleza kwamba pamoja na kwamba alikuwa mahututi, kwa sasa anaendelea vema baada ya kupata matibabu. Hatua inayofuata inaelezwa ni kumpima akili yake baada ya kuonekana akitaka kujaribu kama ambavyo Sura ya 6 ya Kitabu cha Danieli inavyoeleza namna Danieli alivyokuwa na simba bila madhara yoyote. 

Naye akadhani huenda wale simba watakuwa kama paka wake wa nyumbani. Baba mzazi wa Franco ameoneshwa kushtushwa na tukio hilo, ambalo hajui mwanzo wake ulikuwajekuwaje. Huku wazazi waliokuja na watoto wao wakisikitikia kitendo hicho, ambapo walichoweza kufanya ni kuwaziba watoto macho yao ili wasishuhudie mtu akifa kikatili. 

Soma: Mwigizaji 'kajala Masanja' Aamua Kuokoka Na Kumrudia Mungu.

Hata hivyo kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari nchini Chile, inaelezwa kwamba mwisho wa dunia ni sababu mojawapo ya kijana huyo kutaka kuyamaliza maisha yake, kulingana na ujumbe waliokuta amendika.

Source: Gospelkitaa