May 20, 2016

SIRMBEZI WA YESU OKOA MITAA KUACHIA WIMBO MPYA.

Rapper SirMbezi kutokea Yesu Okoa Mitaa ameweka wazi kuwa ataachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Maisha ya Wokovu siku ya tarehe 25/05/2016 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii. 

Rapper huyo pia amebainisha kuwa atauzindua wimbo huo rasmi kwenye tamasha la usiku wa Gospel HipHop litakaolafanyika usiku wa ijumaa ya tarehe 27/05/2106 katika kanisa la T.A.G Tabata, Segerea Chama kwa Mchungaji Bonventure Katembo kuanzia saa tatu kamili usiku na kuendelea.

Wimbo huo ambao amemshrikisha rapper mwingine anayejulikana kama Chief Hope na kufanyika kwenye studio za Home Town records. Baada ya kimya cha mwaka mmoja na nusu bila kuachia kazi yoyote na hii ndio kazi ya kwanza ya SirMbezi kwa mwaka 2016. 

SirMbezi ameweka wazi kuwa kimya chake kilisababishwa na majukumu ya kazi na kitaaluma na kiuahidi kuwa amejistiri kuhakikisha kazi hii mpya inafika mbali. Pia SirMbezi amewashukuru wadau mbalimbali wanaotoa support

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.