May 3, 2016

Askofu Job na Fred Msungu watoa ushauri juu ya wakristo na kashifa za watumishi wa Mungu.

Kupitia account yake ya facebook Askofu Job Mkama Alisema "Kuna habari imeenea kwenye mitandao ya kijamii ya na baadhi ya magazeti kwamba Baba Askofu Dr. Alex Marasusa wa kanisa la KKKT (DMP) ameshikwa ugoni! Binafsi nilizisoma taarifa hivi kwenye gazeti na kuzipuuza kwa msingi wa kwamba Biblia imekataa kukubali mashitaka ya kiongozi unless uwepo ushahidi dhahiri wa zaidi ya MTU mmoja!"

"Niwaombe wakristo wote kote nchini kujiepusha na ushabiki wa kashfa zinazotolewa kwa watumishi wa Mungu bila kujali wanatoka madhehebu gani! Wakristo tujifunze kuwalinda watumishi wa Mungu kwa kuwakemea na kuwapuuza watu wanaotuletea taarifa zenye lengo la kuharibu kanisa!Shetani hawezi kukuletea taarifa njema zinazolihisu kanisa na watumishi wa Mungu! Ulimwengu hauwezi kutamani kuliona kanisa likisonga mbele! Wakristo tulilinde kanisa na viongozi wake kwa nguvu zetu zote! Wakitenda dhambi kanisa linazo taratibu za kuchukua dhidi yao! Asanteni!" aliandika Askofu Mkama.
Katika post hiyo Ndugu Fred Msungu naye ali-comment na kuongezea kwamba "Natamani ujumbe huu uwe ni kwa watumishi wote, si wachache tu...!hata yale matusi ambayo hua anatukanwa Askof Gwajima Na Kakobe wakristo tusingekua tunakua Wa kwanza kushabikia Na kusambaza pengine tusingefika hapa, mwili Wa Kristo unahitaji kuja pamoja tena (YOHANA 17:11)"


Tujiulize Kwanini wanaandika..?Wenzetu waislamu likitokea habari ya Shehe au kiongozi wao kushutumiwa kwa jambo hauta ona wao wakibishana kwenye mitandao ya kijamii Na kusambaza.....Lakini sisi wakristo tuliowengi likitokea habari kama hiyo...ili mradi tu si mchungaji Wa kanisa lako, basi utaisambaza Na kila mtu atahukumu kadri awezavyo, kama tuliweza kuwachafua wengine Na waandishi wakaona tumenunua sana magazeti..hawachaacha
Ifike wakati tusiangalie nani au sura ya mtu ...mtumishi yoyote anaetambulika kwa mwavuli Wa ukristo akichafuka ni kanisa lote limechafuka bila kujali dini ya mtu...TUKIELEWA HILI TUTAHESHIMU NA KUTUNZA THAMANI YA IMANI YETU.YOHANA 17:11" aliandika Ndugu Msungu.